Muhammadu Buhari Ammwaga Goodluck Jonathan Nigeria

Aliyekuwa Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameshindwa katika uchaguzi mkuu nchini Nigeria. Mpinzani wake Generali Buhari ndiye aliyeshinda katika uchaguzi huo kwa kura za wananchi hivyo kufanya chama tawala People's Democratic Party (PDP) kupoteza nafasi hiyo ya kuliongoza Taifa la Nigeria.

Hata hivyo duru zinasema kuwa kushindwa kulidhibiti kundi la Boko Haramu inaweza kuwa sababu kubwa ya Goodluck kushindwa kwa maana alionekana kukaa kimya na kuonesha kushindwa kwa jeshi la serikali .

Maisha ya wananchi wa Taifa hilo yamekuwa hatarini kwa muda sasa na kusababisha  watu  zaidi ya milioni tatu kutoroka makwao na watu zaidi ya 20000 kuuawa.

Muungano wa viongozi wa upinzani chini ya nembo ya chama cha All Progressives Congress (APC)kuliwasaidia kukusanya kura zote na kumfanya Buhari kuibuka na ushindi katika ucxhaguzi huo.


No comments