Makamu wa Rais Burundi, Gervais Rufyikiri atoroka nchini humo
Gervais Rufyikiri, Makamu wa pili wa Rais nchini Burundi ametoroka nchini humo baada ya Kusema kuwa Piere Nkurunziza kugombea muhula wa tatu ni kukiuka katiba na sheria.
Aliyasema hayo katika kituo cha luninga cha France24 na kupinga hatua hiyo ya Nkurunziza.
Hata hivyo msemaji wa serikali ya Burundi amekanusha madai hayo na Kusema kuwa makamu huyo ameenda nje kikazi na kama ametoroka ana sababu zake binafsi.
Viongozi ambao wamekuwa wakipinga hatua ya Nkurunziza wamekuwa wakitoroka kwa kuhofia usalama wao. mapema makamishna wa tume huru ya uchaguzi na jaji mmoja wa mahakama ya kikatiba walitoroka na sasa wanafuatiwa wa Makamu wa Rais.
Kumekuwa na mgogoro mkubwa nchini Burundi kuhusiana na Rais wa nchi hiyo kutaka kugombea muhula wa tatu wa kuliongoza taifa hilo ambao ni kinyume na katiba.

No comments