Mawaziri wa zamani Tanzania Wahukumiwa Kwenda jela

Mawaziri hao Walikuwa na kashfa  ya kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza bila kufuata kanuni na kulisababishia taifa hasara.

Hukumu hiyo imetolewa katika mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam Dhidi ya aliyewahi kuwa waziri wa fedha Basil Mramba na aliyewahi kuwa waziri wa nishati na Madini Daniel Yona wote wamehukumiwa miaka mitatu jela ambapo watatumikia kifungo hicho katika gereza la keko.

Basil Mramba alikutwa na hatia katika mashitaka 11 yaliyokuwa yakimkabili ikiwa mashtaka 10 yalikuwa ni ya matumizi mabaya ya madaraka na shitaka la 11 likiwa ni kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11. 7 wakati akiwa madarakani.

Daniel Yona aliyekuwa Waziri wa nishati na Madini, naye amehukumiwa  kwa makosa matano ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara serikali.

Hata hivyo mtuhumiwa wa tatu  Mgonja aliyekuwa Katibu mkuu wa zamani wizara ya  fedha ameachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutoa ushahidi wa kutosha.

Kesi hii ilidumu kwa mda wa miaka saba Huku raia wa nchi hiyo ya Tanzania wakisubiri kuona nini kitaendelea ukizingatia nafasi walizowahi kuwa nazo watuhumiwa hao.


No comments