Mlipuko Afghanistan waua watoto kumi
Mlipuko mkubwa umetokea nje ya kituo cha
kusambaza gesi katika mji wa Herat nchini Afghanistan, ambao umesababisha vifo
vya watoto kumi na mtu mzima mmoja.
Kwa mujibu wa Msemaji wa hospitali amesema watu wengine 18 wamejeruhiwa katika eneo hilo ambalo hutumika kama kambi ya wakimbizi.
Picha katika mitandao ya kijamii inaonyesha miale ya moto juu angani japo bado haijabainika iwapo mlipuko huo ulikuwa ajali , au shambulio.

No comments