MITUMBA KUZUIWA AFRIKA MASHARIKI
Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokutana jana mjini Arusha, Tanzania wameamua kupiga marufuku uagizaji wa nguo na viatu kuu vya mitumba.
Utekelezaji wa azimio hilo la kutoingiza mitumba utaanza kutekelezwa baada ya miaka mitatu..
Lengo la marufuku hiyo ni kwaajili ya kuinua viwanda vya bguo katika kanda ya Afrika Mashariki.
Serikali za Afrika Mashariki zimekuwa zikilaumu uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika kama moja ya sababu zinazofanya viwanda vya nguo na ngozi kusambaratika na hivyo kuwanyima wenyeji nafasi ya ajira.

No comments