BABU SEYA HURU KWA MSAMAHA WA RAIS

Msanii wa muziki nchini Tanzania Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na Mwanaye Papi Kocha ni miongoni mwa wafungwa watakaoachiwa huru kutokana na msamaha wa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alioutangaza leo katika maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya uhuru wa Tanganyika (sasa Tanzania).

Msamaha huo unawahusu wafungwa 8218 ambapo 1889 wataachiwa huru huku wafungwa 6329 wao watapunguziwa muda wa kukaa gerezani.

Wafungwa 61 kati ya hao ni wale waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Babu Seya na wanaye watatu walihukumiwa kifungo cha maisha gerezani mnamo mwaka 2004 katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto ambapo baadaye baada ya rufaa wawili walitoka hivyo kubaki yeye na mwanaye mmoja maarufu kama pipi kocha.

No comments