Wanajeshi wa Tanzania wauawa Congo DRC


Takribani Wanajeshi 14 wanaolinda amani nchini Congo chini ya mpango wa umoja wa mataifa wameuawa huku wengine 53 wakijeruhiwa baada ya kambi yao kuvamiwa na waasi. Umoja wa mataifa umethibitisha kuwa 12 kati ya waliouawa ni kutoka Tanzania.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres ameshutumu vikali shambulio hilo huku akiitaka Congo kufanya uchunguzi ili kunaini waliohusika na sambulizi hilo na kuongeza kuwa kitendo hicho ni sawa na uhalifu wa kivita.

"Ningependa kueleza kusikitishwa kwangu na shambulio hilo lililotekelezwa usiku wa kuamkia jana dhidi ya walinda amani wa umoja wa mataifa nchini Congo" alisema Bwana Guterres


Kwa mujibu wa umoja wa mataifa, waasi wa ADF (Allied Democratic Forces) ndiyo wanaonyooshewa kidole kuhusu kutekelezwa kwa shambulio hili baya kuwahi kutokea miaka ya hivi karibuni. ADF ni kundi la waasi ambao chimbuko lao ni Nchini Uganda lakini waliingia Congo na wamekuwa wakituhumiwa kufanya vitendo vya kikatili katika maeneo mbalimbali nchini Congo.

Vikosi zaidi vimetumwa katika kambia ya Jeshi ya Semuliki eneo la Beni mkoa wa kivu kaskazini kwaajili ya kuangalia hali zaidi na kusaidia kuharakisha huduma kwa majeruhi.

Umoja wa mataifa una wanajeshi kutoka katika mataifa mbalimbali amabao huepelekwa kulinda amani katika maeneo yaliyo na hali mbaya ya kiusalama.



No comments